This archive report was first published on 4 December 2019.
Chuo Kikuu cha Daystar kilikuwa katika kisasi baada ya transfoma kulipuka karibu na maeneo ya kuegesha magari mwendo wa saa kumi unusu Jumatano, Disemba 4, 2019.
Maafisa wa usalama katika chuo hicho walitoa taarifa kwamba kisa hicho kilishughulikiwa kwa muda ufaao, na hakuna maafa yaliyoripotiwa.
"Hakuna maafa yaliyoripotiwa, lakini gari la mmoja wa wanafunzi liliteketea kwenye mkasa huo," alisema Mkuu wa usalama wa chuo hicho, Steve Leakono.
Kenya Power bado haijatoa taarifa kufikia sasa kuhusiana na kisa hicho.