Skip to main content

Omosh, Muigizaji wa Tahidi High, Ashukuru Mungu baada ya Kuponea kwenye Ajali

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 4 December 2019.

Muigizaji wa kipindi cha Tahidi High, Omosh, alihusika kwenye ajali ya barabarani lakini akaponea bila majeraha yoyote. Alisema alihusika kwenye ajali hiyo pamoja na DJ Patchez na mkewe.

Kulingana na ripoti kwenye ukurasa wa Facebook wa DJ Patchez, wawili hao pamoja na mkewe walikuwa wakitoka kwenye harusi wakati ambapo ajali hiyo ilifanyika. Gari lao lilipata uharibifu mkubwa lakini hakuna mtu aliyejeruhiwa.

DJ Patchez alisema aligongana na gari lililokuwa mbele yake kutokana na mvua kubwa iliyozuia mtu kuona vizuri. Mke wangu alikuwa ameketi kando yake na Omosh kiti cha nyuma. Mikanda ya usalama ilitusaidia sana.

Omosh alihusika kwenye ajali ya barabarani. Picha: The Insyder

" Nilipata ajali mbaya ya barabarani nikiwa na mke wangu pamoja na 'Omosh' wa Tahidi High. Gari langu liliharibika kabisa lakini kwa neema zake Mungu tuliepuka salama. Maombi hufanya kazi," Patchez alisema.

Ajali hiyo ilifanyika mnamo Jumapili, Disemba 1.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →