This archive report was first published on 3 December 2019.
Madini ya protini na chuma katika senene ¶
Senene ni wadudu ambao wana madini ya protini, chokaa na chuma, na wana patikana kwa wingi nchini Uganda, Tanzania, na Rwanda.
Wadudu hao wana patikana kwa wingi katika maeneo ya Kagera, Bukoba nchini Tanzania, na Masaka katikati mwa Uganda.
Joseph Babyekangaba, mkazi wa Jinja, Uganda, anasema kuwa amewala senene tangu alipozaliwa miaka thelathini iliyopita.
"Hawa wadudu tumewala kijijini tangu nilipozaliwa na bado wanaliwa huko na hata hapa mjini, sidhani kufikia sasa kama kuna jamii hapa ambayo haifurahii kula senene," Babyekangaba alisema.
Senene huliwa kwa vyakula vingine kama vile sima, pia huweza kuchanganywa na vyakula vingine au kuliwa pekee.
Wakati wa msimu wa wadudu hao, kila sehemu utaona watu wakiweka mitego yao kuwakamata, na zoezi hilo hufanywa usiku na ni lazima kuwapo mwangaza wa kutosha ili kuwavutia.
Senene ni muhimu katika kuziba pengo la uhaba wa chakula, na Ripoti ya Shirika la Chakula na Kilimo (FAO) ya 2013 iliwataka watu kuongeza wadudu katika chakula chao.
Idadi ya wadudu inayowala ni karibia watu bilioni, na inazidi kuongezeka kila mwaka.