Skip to main content

Cyrus Oguna: Wakenya Wanunue Matanki ya Maji Kama Zawadi ya Krismasi

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 3 December 2019.

Wakati wa mvua kubwa inayoendelea kunyesha nchini, Msemaji wa serikali Cyrus Oguna amewarai Wakenya wanunue matanki ya maji ili waweze kuteka maji yanayotokana na mvua kubwa.

Amesema kila Mkenya anastahili kuwajibika angalau amnunulia mzazi wake tanki la maji kama zawadi ya krismasi.

"Kwa mwezi huu wa krismasi, tafadhali wajibikeni angalau muwanunulie mama zenu matanki ya kuhifadhi maji, hii itakuwa kama zawadi ya krismasi," Oguna alisema.

Watu 123 wamepoteza maisha na wengine 17,000 wakiachwa bila makazi kufuatia mvua kubwa inayoendelea kunyesha nchini.

Matanki hayo yatahifadhi maji yatakayotekwa kutokana na mvua kubwa inayoendelea kunyesha katika sehemu mbali mbali za nchi.

Watu 300,000 wameathiriwa na mafuriko hasa kutoka katika kaunti 10.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →