Skip to main content

Serikali Kugharamia Matibabu na Mazishi ya Waathiriwa wa Maporomoko ya Ardhi Pokot

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 3 December 2019.

Maporomoko ya ardhi katika kaunti ya Pokot Magharibi yalikuwa na madhara makubwa kwa watu wengi, na serikali ya Kenya imeahidi kugharamia matibabu na mazishi ya waathiriwa.

Watu 43 walifariki kufa baada ya kusombwa na mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa inayoendelea kunyesha sehemu kadhaa za nchi.

Maporomoko hayo yalikuwa na madhara makubwa kwa watu wengi, na serikali ya Kenya imeahidi kugharamia matibabu na mazishi ya waathiriwa.

Wakati wa kujibu maswali kuhusu maporomoko hayo, Kamishna wa kaunti ya Pokot Magharibi Apollo Okello alisema afisi yake inashughulikia mipango ya mazishi ya watu 43 waliofariki kutokana na maporomoko hayo.

Okello pia alisema serikali ina mpango wa kuwapa makazi zaidi ya waathiriwa 4,000 ambao nyumba zao zilisombwa na mafuriko.

Awali gavana wa Pokot Magharibi John Lonyangapuo alikuwa ametangaza kuwa watu 58 ndio walipoteza maisha, madai ambayo serikali imekana na kusisitiza ni watu 43 waliofariki.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →