This archive report was first published on 3 December 2019.
Bomet: Nusra Polo Aachwe na Gari Akichovya Asali Kwenye Gesti ¶
Sherehe ya harusi ilikuwa kwenye eneo la Sotik, kaunti ya Bomet, mnamo Desemba 3, 2019.
Jamaa alipigwa simu na aliposhika alidai kuwa alikuwa karibu kufika kwa basi, lakini dereva alikataa kugusa gari ili waondoke.
Wakati sherehe ikiendelea, jamaa alipatana na mrembo ambaye walijuana tangu zamani na wawili hao wakaamu kufufua mahaba ya awali.
“Jamaa alimuomba demu amrambishe asali akisema hiyo ilikuwa nafasi yao ya kipekee. Lakini kipusa alichukua muda kujibu ombi hilo kabla ya kumkubalia jombi kukata kiu,” mdaku alisimulia.
Wasafiri walianza kumshinikiza dereva kungurumisha gari ili waondoke baada ya kuchoka kumsubiri barobaro ambaye alikuwa anawachelewesha, naye dereva hakusita kufanya hivyo.
“Lakini hatua chache tu polo alionekana akikimbia mbio huku anapiga kelele asiachwe. Kilichowafanya watu kuangua kicheko ni polo kuonekana akifunga zipu huku akijaribu kukimbia kufikia basi,” mdaku alisimulia.