This archive report was first published on 2 December 2019.
Waziri wa Michezo Amina Mohammed alikuwa na wakati mgumu kuhutubia umma wakati wa Koroga Festival iliyoandaliwa katika ukumbi wa Bomas siku ya Jumapili, Desemba 1, 2019.
Alipanda kwenye jukwaa kutoa hotuba yake kwa wananchi ambao walikataa kumuazima sikio.
Sherehe ya Koroga Festival ni hafla ya kufurahia miziki ya Kiafrika, chakula, usanii na mtindo wa mavazi.
Waziri Amina Mohammed alikuwa anawakilisha serikali katika hafla hiyo ya Koroga, na alipata mzozo wakati wa kuhutubia umma.
Umati ulianza kuzua huku wengine wakisema "aende uko".
"Najua sipaswi kuhutubu leo kwa sababu tuko hapa kujifurahisha, tunajifurahisha ama sivyo?" waziri huyo alisikika akisema kabla ya kuzomewa na umati wenye hamaki.
Changamoto kuu ya Wizara ya Michezo ni kukosa kuwatambua wanaspoti wa Kenya na pia kuhangaika kila mara kwa wanariadha na wanasoka ambao wamekuwa wakiwakilisha taifa hili katika mashindano tofauti huku wakikosa tiketi za kusafiri na pia malazi.