This archive report was first published on 1 December 2019.
Waziri wa Usalama wa Ndani Fred Matiang'i amekuwa katika kikwazo baada ya Mbunge wa Kikuyu Kimani Ichung'wa kumtaka kukamata wabunge wa Tangatanga.
Ichung'wa alisema Matiang'i anatumia nafasi yake kama waziri kuwahangaisha wanasiasa wanaoegemea upande wa Naibu Rais William Ruto.
Alisema Matiang'i amehusishwa na sakata humu nchini na anawanyoshea wengine kidole tu.
"Huyu Matiang'i amekuwa akinufaika na fedha kutoka sakata ya shamba la Ruaraka na sasa anatuambia hatakubali ujinga, lakini tunamwaambia sisi pia ni wanaume na hatutaki ujinga pia," alisema Ichung'wa.
Ichung'wa aliongeza, "Sasa kwa sababu uko na maafisa wa polisi, kuja utukamate, ukiweza hata tumeze lakini hatutoki kwa kundi la hustler,".
Waziri Matiang'i amedaiwa kutumia wadhifa wake kuwahangaisha wanatangatanga.
Mapema mwaka huu, Matiang'i aliwaondoa maafisa wa polisi wa wabunge wa Tangatanga.