This archive report was first published on 30 November 2019.
Familia moja ya Makueni imeachwa na mshtuko baada ya kifo cha mfanyabiashara Mumo Ngewa ambaye alifariki kwa njia ya kutatanisha.
Mumo aliondoka nyumbani mwake katika kijiji cha Kalawa kuelekea safari ya biashara eneo la Athi River mwanzoni mwa wiki lakini kulingana na mkewe mwili wake ulipatikana ndani ya chumba cha kulala kilichoko kwenye barabara ya Mombasa-Nairobi.
Mwili wa marehemu ulipelekwa katika makafani ya hospitali ya Shalom ambapo upasuaji wa maiti ulifichua alifariki baada ya kula sumu.
Mjane Rose Mumo alizungumza na NTV Ijumaa, Novemba 29, na kusema alizungumza kwa muda na mumewe jioni hiyo majira ya saa moja jioni.
Rose alisema alizungumza na mumewe na kumwaridhia kwamba alikuwa amekodi chumba cha kulala kwenye barabara ya Mombasa-Nairobi ambapo mwili wake ulipatikana.
Marehemu alikuwa amedungwa kisu mara kadhaa kifuani na shingoni ingawa upasuaji wa maiti ulionesha alifariki baada ya kula sumu.