This archive report was first published on 30 November 2019.
Naibu Rais William Ruto alikabiliwa na hali ngumu wakati wa uzinduzi wa BBI mnamo Jumatano Novemba 27, 2019, ambapo alidhalilishwa vibaya na maafisa wa usalama wa Rais Uhuru Kenyatta.
Wafuasi wake wanasema kulikuwa na njama kubwa iliyopangwa na upinzani pamoja na baadhi ya maafisa wa serikali kuhakikisha kuwa wanamuabisha DP.
Kitumbua kilianza kuingia mchanga baada ya DP kufungiwa nje ya mkutano wa Rais Uhuru Kenyatta, Raila Odinga na viongozi wengine katika eneo la wageni waheshimiwa.
Imewauma sana wandani wake kuwa kiongozi wa haiba ya naibu rais alizuiwa kuingia kwenye chumba hicho na badala yake akatakiwa kusimama nje ya mlango asubiri mazungumzo yaliyokuwa ndani yaishe.
Video ya DP Ruto nje ya mlango huo, huku mmoja wa maafisa wa usalama akimzuia kuingia, imekuwa kama mwiba kwa wafuasi wake.
DP Ruto alionekana kama mtu aliyekuwa na mawazo mengi sana wakati wa uzinduzi wa BBI.
Alionekana kama mtu aliyekuwa akijiuliza maswali ya ni lini hafla hiyo itakamilika.
Wakati wote Ruto alionekana kama mtu aliyekuwa akijiuliza maswali ya ni lini hafla hiyo itakamilika.