This archive report was first published on 29 November 2019.
Seneta wa Elgeyo Marakwet Kipchumba Murkomen alimuonya kinara wa ODM Raila Odinga kuhusu hatua ambayo BBI imepiga kwani msema ukweli atakuwa ni bunge.
Alipochapisha jumbe kwenye Twitter, Murkomen alimuonya Raila dhidi ya kujivuna kuhusu hatua ambayo BBI imepiga kwani ni bunge tu ambalo litatoa uamuzi wa mwisho.
Alisema, "Ningependa kumshauri Odinga na kikosi chake kuisoma ripoti ya BBI kabla ya kutoa maoni. Ripoti hiyo inategemea bunge kutoa mwelekeo kikamilifu ikiwemo pia kura ya maamuzi."
Alipochapisha jumbe zake alizozichapisha Alhamisi, Novemba 28, Murkomen alimuonya Raila dhidi ya kujivuna wakati bunge ndilo litakalotoa uamuzi wa mwisho.
Chama cha Jubilee kilishinda viti 141 kati ya 290 katika bunge, na kufuatwa na ODM ambayo ilinyakua viti 63, kisha Wiper na viti 20 huku vyama vingine vya muungano wa NASA vikijishindia nafasi 34 katika uchaguzi mkuu wa 2017.
Wakati wa uzinduzi wa BBI Jumatano, Novemba 27, kiongozi huyo wa wengi alizua kizaazaa baada ya kudai kuliwepo na njama ya kuwazima viongozi wenye maoni tofauti kuhusiana na ripoti hiyo.