This archive report was first published on 29 November 2019.
Mchekeshaji maarufu na mtangazaji wa stesheni ya redio ya Nation FM, Oga Obinna amesherekea siku ya kuzaliwa ya mpenzi wake kwa njia ya kipee.
Obinna alikuwa na bashasha na alikuwa akiandika ujumbe mrefu kwenye ukurasa wake wa Instagram, kumumiminia sifa chungu nzima mpenziwe huku akiwa amenunulia gari la aina ya Toyota Note.
Obinna alisema mpenziwe anapenda sana magari na hangekosa kumfurahisha na aina ya gari ambalo amekuwa akilimezea mate.
Alisema pia mpenziwe amekuwa akiwalea watoto wake bila ubaguzi ikizingatiwa amejaliwa na wanawake tofauti.
Obinna yuko na watoto wanne, kila mmoja akiwa na mamake.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.