This archive report was first published on 28 November 2019.
Mihemko ya Video ya Twa! Twa! na Taarifa Zingine Zilizotamba Wiki Hii ¶
Wiki hii, TUKO.co.ke inakupakulia kwa mukhtasari matukio na habari muhimu zilizogonga vichwa vya habari ili ukapate kufahamu kwa upana na utendaji mambo yalivyo ulimwenguni.
Novemba 27, 2019
Seneta Kipchumba Murkomen alikamatwa na kisasa kwenye mkutano wa BBI. Matamshi yake yalizua hali tete huku baadhi ya waliokuwepo kwenye hafla ya uzinduzi wa ripoti ya BBI wakimkemea na wengine kumuunga mkono.
Alhamisi, Novemba 27, 2019, Msimamizi wa Maabara ya Serikali Joseph Kimani alisema matokeo ya DNA ya mwanamume asiyejulikana ilipatikana kwenye kamba ambayo ilitumika kumfunga Monica Kimani.
Novemba 27, 2019, Dennis Itumbi alikamatwa na kisasa kwenye mkutano wa BBI. Alisukumwa kwenye jukwaa kuu katika ukumbi wa Bomas of Kenya wakati wa uzinduzi wa ripoti ya Jopo kazi la Maridhiano (BBI).
Novemba 27, 2019, Mke wa pasta alisema, ngono ndio mchezo wa pekee ambao Mungu aliutengeneza. Alisema hilo katika video iliyosambaa mtandaoni.
Novemba 27, 2019, Jaji Mkuu David Maraga alisukumwa nyuma ya jukwaa kuu katika ukumbi wa Bomas of Kenya wakati wa uzinduzi wa ripoti ya Jopo kazi la Maridhiano (BBI).
Novemba 27, 2019, takriban watu 30 walifariki kutokana na mvua kubwa ambayo imenyesha na kusababisha maporomoko ya ardhi kaunti ya Pokot Magharibi.
Novemba 27, 2019, afisa wa polisi ambaye anahudumu kaunti ya Mombasa alipatikana ameaga dunia ndani ya baa abapo alikuwa akijivinjari kwa mvinyo.
Novemba 28, 2019, chama cha ODM kinahamia ofisi mpya ambazo zinafunguliwa Alhamisi, Novemba 28. Ofisi hizo katika jumba la thamani ya zaidi ya KSh 150 milioni, ndio makao makuu mapya ya chama hicho.
Novemba 27, 2019, majibizano makali yaliibuka kati ya mbunge wa Gatundu Kusini Moses Kuria na mwakilishi wa kina mama kaunti ya Homa Bay Gladys Wanga kuhusu ripoti ya BBI.
Novemba 27, 2019, mwanamke mmoja Mkenya anayeishi nchini Marekani, anakabiliwa na mashtaka ya kujaribu kuwahonga maafisa wa polisi baada ya kupatikana akiwa mlevi na kugongesha gari lake.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.