This archive report was first published on 27 November 2019.
Siaya: Polisi Wadaiwa Kukataa Kumshtaki OCS Kwa Mauaji ¶
Polisi wamegunduliwa kukataa kumshtaki OCS Sabina Kerubo kwa mauaji ya mwanahabari Eric Oloo, kwa mujibu wa Kamishna wa Siaya Michael ole Tialal.
Eric Oloo alipatikana ameuawa nyumbani kwa OCS Sabina Kerubo huko Ugunja, Siaya, na familia yake inasema kuna njama ya polisi kukataa kumshtaki mwenzao kwenye kesi hiyo.
Wawili hao walikuwa wakichovya buyu la mapenzi kabla ya mambo kuenda kinyume, na mwanahabari Oloo alipatikana ameuawa nyumbani kwa OCS Kerubo.
Michael ole Tialal, Kamishna wa Siaya, amesema kuna mpango wa kuhakikisha OCS Sabina Kerubo hashtakiwi kwa mauaji ya mwanahabari Eric Oloo.
“Nimegundua polisi wananidanganya. Niko na habari za ujasusi kuwa mshukiwa Kerubo anapangiwa kutumika kama shahidi wa upande wa mashtaka na ndio sababu hajakamatwa,” alisema Tialal.
Aliongeza, “Sipendi mchezo huu wa paka na panya ambao polisi wanacheza katika kujaribu kuzuia mwenzao kukabiliwa kisheria.”
Eric Oloo alipatikana ameuawa nyumbani kwa OCS Sabina Kerubo, na familia yake inasema kuna njama ya polisi kukataa kumshtaki mwenzao kwenye kesi hiyo.