Skip to main content

Wakenya wampongeza Musalia Mudavadi kwa hotuba yake kuhusu BBI

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 27 November 2019.

Hotuba ya Musalia Mudavadi kwenye hafla ya uzinduzi wa ripoti ya BBI ilimpongeza na kujenga imani kwa wakenya wengi.

Alionekana kujiandaa vema kwa hotuba hiyo, akizungumzia suala kuu kuwaliko viongozi wengine waliozungukia kwenye masuala ya kisiasa.

Alisema ajenda kuu ya BBI sio kuhusu uzinduzi wa wadhifa wa waziri mkuu, bali ni kuwaunganisha Wakenya.

"Tunataka kufanya maamuzi yatakayo faidi kila Mkenya katika nyakati zijazo, lazima tuelewane ili tujenga Kenya yetu, kila Mkenya yuko na haki ya kutoa kauli kuhusiana na ripoti hii ya BBI, hebu na tuwe waangalifu tunapozungumzia mchakato huu," Mudavadi alisema.

Alipiga kifungu kwa wale viongozi ambao hawataki kusoma ripoti hiyo, kwa sababu wandani wao hawajaisoma.

"Hebu na kila mtu ajitolee kusoma ripoti hiyo na atoe uamuzi utakaomfaa, sio eti ukose kuisoma kwa sababu Musalia Mudavadi hajaisoma," Mudavadi aliongeza.

Aliongeza, "Hebu na tusiifanye ripoti hii kuwa ya kisiasa, mnafanya ionekane ni kuhusu kugawana nyadhifa, itakuwaje na suala ya uchumi?,mbona sasa tusiwape motisha watumishi wa umma?"

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →