This archive report was first published on 26 November 2019.
Waziri wa Usalama wa Ndani Fred Matiang'i alishindwa kufika kaunti ya Pokot Magharibi kuwatembelea waathiriwa wa mkasa wa maporomoko ya ardhi, kwa madai ya kuwepo kwa hali mbaya ya anga.
Madai hayo yalikuwa ya kipekee kwa sababu ndege ya Naibu Rais William Ruto ilipitia eneo hilo na kuwatembelea waathiriwa.
Wabunge wa Rift Valley wamedai Matiang'i alikuwa na haja ya kuhudhuria mkutano wa BBI wala hakutaka kuwatembelea wananchi wa kawaida waliathirika na maporomoko ya ardhi.
Wabunge hao wakiwemo mbunge wa Pokot Kusini David Pkosing walidai Matiang'i ameupa kipaumbele mpango wa BBI na kusahau maisha ya mwananchi wa kawaida.
"Inasikitisha sana kuwa Naibu Rais William Ruto aliweza kufika Pokot Magharibi kuwatembelea waathiriwa wa mkasa wa maporomoko ya ardhi ila waziri wetu wa usalama hakuweza kwa madai ya kuwepo kwa hali mbaya ya anga, nashangaa sana kwani ndege ya Naibu Rais ilipitia wapi," Pkosing alisema.
Wabunge hao wamedai Raila alimpigia Matiang'i simu na kumuarisha ahudhurie maandalizi ya mkutano wa BBI na ndio sababu kuu alisitisha safari ya Pokot.
Naibu Rais William Ruto na Waziri wa Mipaka Fred Matiang'i wakishuhudia ripoti ya mpango wa BBI iliyowasilishwa kwa Rais Uhuru Kenyatta Jumanne, Novemba 26.