This archive report was first published on 26 November 2019.
Video ya Bernie Sanders akisakata densi huku wimbo mpya wa mwanamuziki Gilad Millo unachezwa kwa lugha ya Kiswahili umesisimua mitandaoni.
Gilad Millo, ambaye ana asili ya Uyahudi, ameishi Kenya kwa miaka kadhaa na sasa ana uwezo wa kuzungumza lugha ya Kiswahili kwa ufasaha.
Wimbo huo, "Sitaki Mwingine", umepokelewa vema na mashabiki wake mitandaoni na hangeweza kuficha furaha yake baada ya kuona mwanasiasa mkubwa wa Marekani akisakata densi kimahaba akiwa amemkumbatia mwanamke.
"Nina furaha tele, hebu mtizame mgombea wa urais nchini Marekani Bernie Sanders anaposakata densi wimbo wangu utapochezwa, kutoka Kenya hadi Marekani, furaha iliyoje?, Gilad aliandika Instagram.