Skip to main content

Mwanga wa Kiswahili: KCPE 2019 yaonesha shule binafsi zinazifukia mchangani zile za umma

N

Nyakundi Report

Newsroom 2 min read

This archive report was first published on 26 November 2019.

Mwanga wa Kiswahili: KCPE 2019 yaonesha shule binafsi zinazifukia mchangani zile za umma

Shule za kibinafsi zilifanya vyema zaidi kuliko zile za umma katika matokeo ya KCPE 2019, kama ilivyotangazwa na Waziri wa Elimu Profesa George Magoha juma lililopita.

Shule mbalimbali na walimu walifurahi na walionekana pia wakisherehekea tuseme ushindi wa wanao. Takwimu zilionesha kuwa shule za watu binafsi zilifanya vyema kuliko za umma.

Waziri wa Elimu Profesa George Magoha alisema kuwa shule za umma zinasema kujitolea kwa walimu na wanafunzi ni sehemu kubwa iliyochangia alama za juu miongoni mwa watahiniwa na kwa jumla matokeo bora.

Walimu katika shule za umma walisema kuwa utiriri wa wanafunzi katika madarasa yao ulichangia matokeo duni. Kwa mfano, kuna shule moja ya umma ambayo ilikuwa na watahiniwa zaidi ya mia saba, na kwa idadi hiyo ni vigumu kushughulikia maslahi ya mwanafunzi inavyofaa.

Wenzao katika shule binafsi, idadi ya wanafunzi haikuzidi thelathini. Matokeo ya KCPE 2019 yalionesha kuimarika kwa alama katika Kiswahili kuliko mwaka jana.

Profesa George Magoha alisema kuwa bora kutaja kujitolea kwa walimu, wanafunzi na bidii ya kila mhusika vilifanikisha matokeo hayo.

Alama za juu katika Kiswahili zilikuwa ishara ya hatua zilizopigwa katika kuhakikisha lugha hii inazidi kuenziwa na wanafunzi wengi katika shule zetu.

Matumaini ya wapenzi wa lugha hii ni kwamba, itaendelea kutamba zaidi na kutangazwa bora zaidi wakati matokeo ya mtihani wa KCPE siku zijazo yatakapokuwa yakitangazwa.

Profesa George Magoha alisema kuwa kumbuka Kiswahili ndio fimbo ya Mwafrika tuitumie.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →