Skip to main content

Polisi wapata kadi 23 za ATM zimefichwa kwenye sehemu za siri za mwanamke ▷ Kenya News

N

Nyakundi Report

Newsroom 2 min read

This archive report was first published on 26 November 2019.

Polisi wapata kadi 23 za ATM zimefichwa kwenye sehemu za siri za mwanamke

Polisi wamepata kadi 23 za ATM zimefichwa kwenye sehemu za siri za mwanamke mwenye umri wa kati ambaye anashukiwa aliziiba kutoka kwa wateja.

Halima Juma, mwanamke mwenye umri wa kati, alikamatwa katika ATM ya benki ya CRDB mtaa wa Mbagala baada ya keshia wa benki hiyo kushuku alikuwa akitekeleza uhalifu.

Halima alipataikana na kadi 23 za ATM kutoka kwa benki tisa tofauti, ikijumuisha CRDB, Equity, Diamond Trust Bank, CFC Stanbic, NBC, NMB, Amana, Posta, na ACB.

Wakati wa msako katika kituo cha polisi, kadi za ATM za benki tisa tofauti zilipatikana ndani ya sehemu yake ya siri.

Halima alisema kwa polisi kwamba alikuwa tayari kuwasaidia watu kutoa pesa kutoka kwa mashine hiyo, lakini alibadilisha kadi za wateja na kuwapea kadi tofauti ambayo ni feki.

Halima alisema kuwa walikuwa wakiwalenga wazee matajiri, wanaume na wanawake wasiojua kusoma, na kujifanya kuwasaidia kutoa pesa kutoka kwa ATM.

Wahalifu hao huingia katika chumba tofauti cha ATM na kutoa pesa hizo huku mteja akiripoti suala hilo kwa benki husika.

Tayari polisi wameanzisha uchunguzi kuhusiana na kisa hicho ili kuwanasa na kuwashtaki wahalifu hao.

Halima alipigwa ripoti na Ernest Mika Sakala, polisi mstaafu, mnamo Oktoba 23, 2019, kwamba alibadilisha kadi yake ya ATM ya Benki ya CRDB na nyingine sawia ya benki hiyo.

Wakati Sakala alikwenda kutoa pesa, alitambua kwamba kadi aliyokuwa nayo sio yake na kufululiza hadi benki hiyo kutafuta ushahuri.

Halima alipatikana na kadi za ATM kutoka kwa benki tisa tofauti, ikijumuisha CRDB, Equity, Diamond Trust Bank, CFC Stanbic, NBC, NMB, Amana, Posta, na ACB.

Halima alipigwa ripoti na Ernest Mika Sakala, polisi mstaafu, mnamo Oktoba 23, 2019, kwamba alibadilisha kadi yake ya ATM ya Benki ya CRDB na nyingine sawia ya benki hiyo.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →