Skip to main content

Kenya News: Daktari Akimbia Kortini Kumshataki Mpango wa Kando

N

Nyakundi Report

Newsroom 2 min read

This archive report was first published on 26 November 2019.

Magazeti ya Jumanne, Novemba 26

Magazeti ya Jumanne, Novemba 26, yameipa uzito ripoti ya BBI inayotazamiwa kukabithiwa hii leo kwa Rais Uhuru Kenyatta na Kinara wa Upinzani Raila Odinga.

Magharibi Pokot, ambapo mkasa ulitokea siku ya Jumamosi, Novemba 23, pia ni taarifa nyingine iliyoangaziwa katika magezeti haya.

Uhalifu wa Daktari

Daktari mmoja amekimbia kortini kumshataki mpango wa kando baada ya kumdhulumu na kumuaibisha mpenzi wake wa zamani.

Alipokea mwanamume huyo kama mgonjwa na kisha baadaye wakaanza uhusiano wa kimapenzi licha ya daktari kuwa katika ndoa.

Alisitisha uhusiano huo mwaka mmoja baadaye lakini mwanamume huyo alianza kumhangaisha kwa kumtumia mumewe, wanawe na wafanyakazi wenzake picha zao wakati walikuwa katika uhusiano.

Madai ya KEMRI

Taasisi ya Kutafiti Matibabu nchini (KEMRI) imekanusha madai kwamba dawa za kupanga uzazi husababisha kuongezeka kwa uzito kwa wanawake.

Mtafiti mmoja kutoka KEMRI, Maricianah Onono, alisema kwamba dawa hizo hazina uwezekano wa kusababisha kuongezeka kwa uzito kwa wanawake.

Onono alisema kwamba kunenepa husababishwa na mambo mengi ikiwemo mtindo wa maisha, chakula na pia kukosa kujitunza.

Uhalifu wa Gavana Sonko

Seneti inapania kufanyia uchunguzi ukumbi wa City kwa madai ya utumizi mbaya wa rasilimali, mzozo wa uongozi na kusitishwa kwa utenda kazi baada ya Gavana Mike Sonko kuwafuta kazi baadhi ya wafanyakazi.

Spika wa Seneti Ken Lusaka aliagiza Kamati ya Ugatuzi na Uhisiano wa asasi za serikali kuchunguza suala hilo na kutoa mapendekezo yake kwa bunge hilo.

Spika huyo alionya kamati hiyo dhidi ya kufanya uchunguzi huo kwa upendeleo na kuweka Bunge hilo katika ramani mbaya.

Uhalifu wa Kebs

Idara ya Kukagua Ubora wa Bidhaa Kenya (KEBS) imekanushwa kwa kuagiza magunia 5,846,000 ya mbolea yaliyokuwa na viwango vya zebaki.

Mkurugenzi Mkuu wa Mashtaka ya Umma Noordin Haji alimfahamisha hakimu Kennedy Cheruiyot kuwa mashahidi watatu watatoa ushahidi wao katika kesi hiyo.

Alipinga Kebs kujiunga katika kesi hiyo ya uhalifu kama upande wa hamu na kesi hiyo.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →