Skip to main content

Mwanahabari Erick Oloo aliuawa Siaya, Mshukiwa Mkuu Akosekana Kortini

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 25 November 2019.

Mwanahabari Erick Oloo aliuawa Siaya

Polisi wameshakamatisha watu watano kuhusiana na mauaji ya Erick Oloo, mwanahabari wa gazeti la The Star, ambaye aliuawa mjini Siaya, Kaunti ya Siaya, Kenya.

Inspekta Mkuu wa Polisi Sabina Kerubo, ambaye nyumba yake kulipatikana mwili wa marehemu, anatarajiwa kortini Jumanne, Novemba 25, 2019.

Washukiwa wawili wanaoaminiwa kuwa katika eneo la tukio usiku wa mauaji hayo waliwasilishwa kortini na polisi kuiomba kuwaruhusu kuendelea kuwazuilia hadi wakamilishe uchunguzi wao.

Victor Lutta na Franckline Lutta, waliwasilishwa kortini mbele ya Hakimu Mkuu Mkazi wa Siaya Geoffrey Ong’ondo ambaye aliruhusu wazuiliwe siku 11 kabla ya kuwawasilisha kortini kujibu au kukataa mashtaka.

Awali TUKO.co.ke ilithibitisha kukamatwa kwa Kerubo baada ya Kamanda wa Kaunti Francis Kooli kusema na wanahabari, na kuwahakikishia kukamatwa kwa inspekta huyo, bintiye na yaya.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →