This archive report was first published on 25 November 2019.
Mwalimu mmoja kutoka kijiji cha Kogana katika kaunti ya Homa Bay aliondoka nyumbani baada ya kusafiri jijini Nairobi kusahisha mtihani wa Darasa la Nane (KCPE) zaidi ya wiki mbili iliyopita.
Moses Odumbe, mwalimu wa Shule ya Msingi ya Kogana katika kaunti ndogo ya Rachuonyo Kaskazini, aliondoka nyumbani kwake mnamo Novemba 8 mida ya saa 5.30 jioni kuelekea Shule ya Sekondari ya Wasichana ya St. George's jijini Nairobi ambapo alikuwa anatazamiwa kusahisha mtihani.
Alielekea katika baraza la mitihani siku ya kwanza na kukosa kurejea, na familia yake ilikuwa na wasiwasi kwa sababu ya kukosa kurejea nyumbani.
Alisalia mteja hata baada ya zoezi la kusahisha kutamatika, na kupitia msaada wa jamaa zake jijini Nairobi, walitembelea Baraza la Mtihani (KNEC) na kufahamishwa kuwa alifika hapo siku ya kwanza lakini hakurejea tena siku iliyofuata.
Waliripoti kisa hicho katika Kituo cha Polisi cha Kendu Bay na Kilimani eneo la Homa Bay na kaunti ya Nairobi mtawalia.