Skip to main content

Gavana Mutua Amtaka DP Ruto Kujiuzulu Mara Moja

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 24 November 2019.

Gavana wa Machakos Alfred Mutua amemlima Naibu Rais William Ruto akidai kuwa anahujumu juhudi za Rais Uhuru Kenyatta kuhusu suala la jopo la maridhiano, BBI.

Alisema hilo Jumamosi, Novemba 23, wakati wa hafla ya kutoa shukrani baada ya mgombea wa Maendeleo Chap Chap kuibuka mshindi katika eneo la Mutonguni.

Alisema Rais na Naibu Rais hawazungumzi kwa sauti moja kuhusu suala la BBI, na kuwa ni picha mbaya.

Alitaka DP Ruto kujiuzulu iwapo haridhishwi na msimamo wa Rais kuhusu BBI.

Alisema, "Ruto ni wazi kuwa anahujumu juhudi za rais na hili linaonyesha picha mbaya. Anafaa tu afanye uamuzi na kujiuzulu,".

Alisema hilo wakati wa hafla ya kutoa shukrani baada ya Musee Mati kushinda uchaguzi wa wadi ya Motonguni kwa tiketi ya chamacha Maendeleo Chap Chap.

Alisema hilo wakati wa hafla hiyo, ambayo ilikuwa ikiongozwa na katibu wa chama cha ODM Edwin Sifuna.

Alisema Sifuna, "Kama Naibu Rais, anafaa amwambie mdosi wake kuhusu maoni yake juu ya BBI, si kuenda akipiga kelele,".

DP Ruto amekuwa katika mstari wa kwanza kusema kuwa BBI isiwe ni chombo cha kisiasa kinachotumiwa kwa ajili ya uchaguzi wa 2022.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →