Skip to main content

KCSE 2019: Mtahiniwa wa KCSE Auliwa na Umati wa Hamaki kwa Kuiba Simu Sokoni

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 24 November 2019.

Mtahiniwa wa KCSE alikuwa akiendelea na mtihani wake wa mwisho wa KCSE wakati alikamatwa na umati wa hamaki baada ya kumaliza mtihani wake wa mwisho wa KCSE siku ya Jumamosi, Novemba 23, jioni katika eneo la Sigalagala, Kaunti ya Siaya, Kenya.

Mtahiniwa huyo, Rodgers Bett, alikuwa mwanafunzi katika Shule ya Upili ya Burendwa na alikuwa amemaliza kufanya mtihani wake wa KCSE ambao ulitamatika siku ya Ijumaa.

Mamake mwendazake, Beatrice Khalenya, alidai kuwa kifo cha mwanawe kilichangiwa na kuhusishwa kimakosa na hajawahi kukashifiwa mbeleni kwa wizi.

"Walimua mwanangu kwa kudai kuwa ni mwizi hiyo sio ukweli. Alikuwa tu amemaliza kufanya mtihani wake wa KCSE na tulikuwa tunamtegemea kuinua familia hii siku za usoni lakini ndoto yake ilikatizwa ghafla. Hatujafurahishwa na kile umati kilimfanyia mtoto wetu," alisema Khalenya.

Kamanda wa polisi wa kaunti ndogo ya Shinyalu, Robert Makuon, alisema mwanabiashara huyo alitambulika kama Makau ambaye alihoji kuwa mwanafunzi huyo alikuwa ameiba simu.

Rodgers alilemewa na majeraha katika Hospitali ya Rufaa ya Kakamega ambapo pia mwili wake umehifadhiwa.

Katika Kaunti ya Siaya, washikadau wa elimu bado wanajikuna vichwa kubaini mbivu na mbichi kuhusu chanzo cha kifo cha mtahiniwa wa KCSE aliyekuwa akifanya mtihani wake.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →