This archive report was first published on 24 November 2019.
Published on November 24, 2019, Gavana Mike Sonko anatakiwa kurudi gerezani kuhudumu kipindi anachodaiwa hakumaliza.
Uamuzi huo unatokana na uamuzi wa mahakama wa Machi 12, 1998, ambapo Sonko alifungwa miezi sita gerezani baada ya kukosa kufika mahakamani katika kesi iliyomkabili.
Stakabadhi za gereza la Shimo la Tewa zinaonyesha kuwa Sonko alifungwa miezi mingine sita kwa kukosa kufika mahakamani katika kesi nambari CF 1727/96.
Alitakiwa kuhudumu kipindi cha miezi 12 katika gereza la Shimo la Tewa lakini akahepa baada ya mwezi mmoja.
Alirushwa katika gereza la Shimo la Tewa ambapo angehudumu vipindi hivyo vya miezi kumi na miwili kuanzia Machi 12, 1998 hadi Machi 11, 1999.
Alipotea gerezani mnamo Aprili 16, 1998.
Uchunguzi wa EACC unateta kuwa kando na kosa hilo la gavana huyo kupotea gerezani, alitoa habari za uongo kwenye fomu za kujieleza ambazo hujazwa wakati wa kugombea viti vya kisiasa.
Alisema uchunguzi huo wa EACC ni njama ya kummaliza kisiasa.