This archive report was first published on 24 November 2019.
Shirika la feri nchini Kenya (KFS) limeanzisha shughuli za kuutafuta mwili wa jamaa ambaye aliruka kutoka kwenye feri ya MV Harambee mpaka Bahari ya Hindi.
Kitendo hicho kilitokea Jumapili, Novemba 24, 2019, na KFS imesema mwanaume huyo alikuwa amevalia shati nyeupe na suruali nyeusi.
Aliporuka, feri hiyo ilikuwa imetoka uoande wa ufuo kuelekea kisiwani wakati ambapo kisa hicho kilitokea.
"Tunadhibitisha kuhusu kisa hicho ambapo leo 1:30 am abiria wa kiume ambaye hajatambuliwa, na ambaye alionekana amezongwa na mawazo, alitoka alipokuwa ameketi na kuruka majini," KFS ilisema kwenye taarifa.
Alama za mawimbi makali yalikatiza juhudi za kikosi cha waokoaji kunusuru maisha ya jamaa huyo.
"Juhudi za kumuokoa hazikufaulu kutokana na mawimbi na giza. Kisa hicho kiliripotiwa kwa polisi wa feri," KFS ilisema.