This archive report was first published on 23 November 2019.
Rais Uhuru Kenyatta atuma Wanajeshi wa KDF kusaidia katika Uokoaji baada ya Mvua Kubwa iliyosababisha Maporomoko ya Ardhi katika Kaunti ya West Pokot ¶
Novemba 23, 2019
Maporomoko ya ardhi yalikuwa na madhara makubwa katika kaunti ya West Pokot baada ya mvua kubwa ilinyesha na kusababisha maporomoko ya ardhi. Kwa mujibu wa taarifa za serikali, takriban watu 37 tayari wamedhibitishwa kufariki kutokana na mvua hiyo kubwa.
Rais Uhuru Kenyatta ameamuru wanajeshi wa KDF watumwe katika kaunti ya West Pokot kusaidia katika shughuli za uokoaji baada ya mvua kubwa iliyosababisha maporomoko ya ardhi. Rais Kenyatta amewataka makamishna wa kaunti kuhakikisha watu wote walio kwenye maeneo hatari wameondolewa ili mkasa kama huo usishuhudiwe kwenye kaunti zingine.
Naibu Rais William Ruto pia alituma rambirambi zake kwa familia zote zilizoathirika na kusema, "Maombi yangu, pamoja na ya nchi yote, ni kwa familia, marafiki na wapendwa wa wote waliopoteza maisha yao. Pokeeni rambirambi zangu."
Waziri wa Usalama wa Ndani Fred Matiang'i alisema tayari ndege za kijeshi pamoja na za polisi zimefika maeneo ya mkasa ili kusaidia juhudi za uokoaji. "Serikali imetuma ndege za jeshi na polisi ili kutoa huduma kwa walioathirika. Juhudi za uokoaji ndio zimepewa kipao mbele," alisema.
Waziri Matiang'i alisema pia kwamba tayari wametuma ndege za kijeshi za zile za polisi kuenda kusaidia hali West Pokot.