This archive report was first published on 23 November 2019.
Mfanyikazi wa Eastmatt Akamatwa Baada ya Kamera Kumnasa Akimchapa Mwenzake ¶
Mfanyikazi wa Eastmatt, Ibrahim Taraiya, amekamatwa baada ya kamera kumnasa akimchapa mwenzake wa kike. Anatakiwa kufika mahakamani Jumatatu, Novemba 25.
Uchunguzi huo ulianza baada ya TUKO.co.ke kuripoti kuhusu unyama wa mfanyikazi huyo dhidi ya mwenzake ambao ulifanyika Jumanne, Novemba 19.
ODPP ilisema, "ODPP ameagiza kukamatwa mara moja kwa Ibrahim Taraiya, mfanyikazi wa duka la Eastmatt, Kajiado kwa kumpiga mfanyikazi mwenzake wa kike. Ibrahim atafikishwa mahakamani, Jumatatu,"
Usimamizi wa duka hilo ulimsimamisha kazi Taraiya huku uchunguzi ukiendelezwa na polisi. Kampuni hiyo ilisema, "Sisi kama Eastmatt tunakashifu kisa hicho na ukosefu wa heshima kwa wafanyikazi haswa akina dada. Aliyehusika amesimamishwa kazi na kisa hicho kuripotiwa katika kituo cha polisi cha Kajiado,"
Wakati uo huo, mshukiwa alisimamishwa kazi mara moja na kampuni hiyo huku usimamizi wa duka hilo ukidokeza kwamba maafisa wa polisi wa Kajiado wamelizamia suala hilo.