This archive report was first published on 22 November 2019.
Patricia Macharia, mwanamke wa miaka 22, alikamatwa na polisi baada ya kutishia kumuua jirani yake, Rose Wanjiru, huku akiwa amejihami kwa kisu. Hii ilikuwa tarehe 21, 2019, nje ya ploti wanayoishi katika eneo la Njiiru, kaunti ya Nairobi.
Patricia alikuwa amemkaba Rose pale ambapo jirani mmoja aliingilia kati na kuwatawanya na akimpokonya kisu hicho. Baadaye, mumewe Rose alimchukua kwa nguvu na kumrejesha chumbani.
Rose alipiga ripoti kwa polisi na kupelekea kukamatwa kwa jirani yake. Patricia alikana mashtaka mbele ya hakimu Heston Nyaga ambaye alimwachilia kwa dhamana ya KSh 10,000.
Kesi hiyo itasikizwa tena Machi 24, 2020.