This archive report was first published on 22 November 2019.
Aliyekuwa mwigizaji wa kipindi cha Machachari Tyler Mbaya, anayejulikana kama Baha, atashirikiana na bintiye msanii Akothee Rue Baby kwenye filamu mpya ya Love Daggers.
Wawili hao wataigiza kwenye filamu hiyo ya mahaba, iliyotayarishwa na Versatile Studios na kuendeshwa na muuundaji filamu maarufu Michael Jones.
Aliyekuwa mwigizaji wa kipindi cha Machachari Baha amekuwa katika uigizaji kwa muda mrefu, lakini kwa Rue hii itakuwa mara ya kwanza kuzamia fani hiyo.
Awali mwanamitindo huyo aliigiza katika filamu fupi na mcheshi MCA Tricky ambaye fununu mtaani zinasema kuwa wanachumbiana.