This archive report was first published on 22 November 2019.
Wafuasi wa DP Ruto wameitisha mkutano na Rais Uhuru Kenyatta baada ya kufaulu kwa mkutano wa Sagana Kenya.
Wanasema Rais Uhuru alianza mkutano na wale wa Mt Kenya na sasa wanataka pia kikao naye.
Wafuasi hao wanataka kujadili suala la Mau pamoja na siasa za 2022.
Magavana, seneta, wabunge na MCAs wamesema wanataka pia kupata kikao na Rais Uhuru.
Seneta wa Kericho Aaron Cheruiyot alisema Rais Uhuru alianza mkutano na wale wa Mt Kenya nyumbani na sasa wanataka pia wao kufanya kikao.
"Ni vizuri Rais alianza nyumbani. Pia sisi tunataka kukutana na yeye," alisema Cheruiyot.
Wafuasi hao wanataka kuhakikisha kuhusu uchaguzi wa urais wa 2022 na mabadiliko ya katiba.