This archive report was first published on 22 November 2019.
Usiku wa manane, mlofa mkono gamu alilazimika kumtafuna samaki wake mkavu baada ya kukosa sembe nyumbani.
Alipowasili nyumbani, alikuwa amebeba samaki aliyekaangwa, lakini hakuna sembe nyumbani.
Alipigwa na butwaa kupata hamna sembe, aliamua kuikaanga samaki yake aunde mchuzi angalau asisakamwe, lakini hapakuwepo na mafuta wala kitunguu jikoni.
Aliamua kumtafuna samaki wake kimya kimya, kwa machungu kwani pia hangemuuliza mkewe chochote kwa kuhofia kupogiwa kelele.
Penyenye zinaarifu kuwa mambo hayakuishia hapo kwani mama aliamua huo utakuwa mtindo wa kila siku ndiposa polo ashike adabu.