This archive report was first published on 22 November 2019.
Jowie Aililia Mahakama Imwachilie Kwa Dhamana, Asema Anaumia Gerezani ¶
Joseph Irungu, alias Jowie, mshukiwa wa mauaji ya Monica Kimani, ameiomba mahakama imwachilie kwa dhamana na kusema anaumia gerezani.
Alisema kuwa anataka kuachiliwa kwa dhamana kama mshukiwa mwenzake Jacque Maribe alivyoachiliwa mnamo Oktoba 30, 2018.
Maombi yake ya kuachiliwa kwa dhamana yamekuwa yakitupiliwa nje kwani mahakama inaamini atahitilafiana na uchunguzi.
Alhamisi, Novemba 21, Jowie alisema kuwa anapaswa kuachiliwa kwa dhamana jinsi mshukiwa mwenzake Jacque Maribe alivyoachiliwa.
"Mshukiwa mwenzangu (Jacque Maribe) aliachiliwa kwa dhamana na hajawahi kosa kuhudhuria vikao mahakamani. Mimi pia naomba nifanyiwe vivyo hivyo," alisema.
Maombi yake ya kuachiliwa kwa dhamana yamekuwa yakitupiliwa nje kwani mahakama inaamini atahitilafiana na uchunguzi.
Novemba 20, ripoti iliyowasilishwa na mkaguzi wa serikali ilimuweka Jowie mahali palipotokea mauaji ya marehemu.
Monica Kimani aliuawa Septemba 2018 na mwili wake ulipatikana chumbani mwake Lamuria gardens mtaa wa Kilimani, Nairobi.