This archive report was first published on 22 November 2019.
Kizaazaa Bungeni: Didmus Baraza Kutishia Kumnyorosha Gladys Wanga ¶
Alhamisi, Novemba 21, 2019, kizaazaa kilishuhudiwa bungeni baada ya wabunge Didmus Baraza wa Kimilili, Gladys Wanga wa Homa Bay, na Esther Passaris wa Nairobi kutupiana cheche za maneno.
Utata ulianza wakati wa mjadala wa ripoti ya kamati ya bunge kuhusu kanda ya video ya ufuska iliyohusu mbunge Fatuma Gedi.
Didmus Baraza alizua kizaazaa bungeni baada ya kutishia kuwa kopi wenzake. Picha: Standard
Kamati hiyo ilitoa ripoti yake na kutaka Gedi achukuliwe hatua na bunge kwa kosa la kufichua hatua ya wachunguzi wa DCI kwa wabunge wenzake.
Baraza alitishia kuwapa kofi wabunge Gladys Wanga na Esther Passaris baada ya kutishia kumnyorosha Wanga.
Baraza alisema, "Bwana Spika nilinde kutokana na Gladys Wanga ambaye anapiga kelele. Bwana Spika, nitamnyorosha huyu dada kwa sababu ananipigia kelele," Baraza alisema.
Passaris naye alikerwa na kuamka huku akimtupia maneno makali mbunge huyo kwa kutishia kumpa kofi Wanga.
Didmus Baraza alitishia kumpa kofi Esther Passaris.
Spika Justin Muturi alituliza hali na mjadala ukaendelea bila sokomoko za watatu hao.