Skip to main content

Wycliffe Kori Achola na Dennis Atitwa Atenya Walikamatwa kwa Kuhusika na Wizi wa Kimabavu

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 21 November 2019.

Wycliffe Kori Achola na Dennis Atitwa Atenya walikamatwa na maafisa wa polisi wanaohudumu katika kituo cha polisi cha Githurai Kimbo mnamo Septemba 2019 kwa madai ya kuhusika na wizi wa kimbavu.

Washukiwa hao walishtakiwa na walizuiliwa katika kituo cha polisi cha Ruiru wakisubiri kusikizwa kwa kesi inayowakabili.

Wakati wa kuwa wakirejea gerezani, Achola alimrukia afisa aliyempeleka msalani kabla ya mwenzake aliyekuwa gerezani kushirikana naye na pamoja wakaanza kumshambulia.

Wycliffe Kori Achola na Dennis Atitwa Atenya wanasemekana walihepa saa chache tu kabla ya kusikizwa kwa kesi yao katika mahakama ya Ruiru.

Maafisa wa polisi wameaza oparesheni kali ya kuwasaka washukiwa wawili wa wizi wa kimabavu ambao walihepa katika kituo cha polisi cha Ruiru.

Washukiwa hao waliotambulika kama Wycliffe Kori Achola na Dennis Atitwa Atenya wanasemekana kutoroka majira ya saa kumi na moja asubuhi kulingana na ripoti iliyoandikwa katika kitabu cha kituo hicho chini ya nambari 14/20/11/2019.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →