This archive report was first published on 20 November 2019.
Gavana wa Kirinyaga Ann Waiguru amesema kuwa ni baadhi ya wanasiasa walio na nafasi kubwa kushinda kiti cha urais 2022.
Waiguru alisema hayo kwenye mahojiano na runinga ya Citizen Jumanne, Novemba 19, 2019.
Aliongeza kuwa hali hiyo imemfanya kupigwa kisiasa sana haswa katika eneo la Mlima Kenya kwani anaonekana kuwa miongoni mwa wale wanaoweza kumrithi Rais Uhuru Kenyatta.
Waiguru alisema kuwa siasa za Kenya zinazidi kugeuka kutokana na mwafaka wa kisiasa kati ya Rais Uhuru Kenyatta na Raila Odinga.
Alisema handisheki itabadilisha siasa kwa kiwango kikubwa na kwa sasa mbinu yake ni kusubiri tu ili ajue uamuzi atakaofanya.
Alipoulizwa iwapo anaweza kusema kwa kweli kuwa hawezi kuchukua nafasi ya naibu rais katika muungano wa kisiasa, Waiguru alisema anaweza kukubali nafasi hiyo.