This archive report was first published on 15 November 2019.
Uhuru Kenyatta alikutana na wanasiasa wa Mt Kenya katika Sagana State Lodge, Ijumaa, Novemba 15, 2019.
Alionekana kumlenga Naibu Rais William Ruto ambaye anapambana kuuwahi urais 2022 na wanasiasa marafiki zake.
Uhuru alisema kuwa hajamtaja mtu kuhusu uchaguzi mkuu ujao ingawa marafiki wa Ruto wamekuwa wakidai aliahidi kumuunga mkono wakati wa kampeni ya 2017.
Alitumia msemo wa lugha ya mama, "Nigetha andu angi matige guka guku gwitu gutua thara wene", ili kusema kwamba hakuwezi kuwa na watu kutoka nje kuvuna nyasi isiyokuwa yao.
Uhuru alisema kwamba litakuwa ni jambo la kusikitisha kwa wanasiasa wa Mt Kenya kutoangalia mutakabali wa eneo hilo, na badala yake kuzama katika siasa chafu.