This archive report was first published on 15 November 2019.
Didmus Barasa, mbunge wa Kimilili, amesema kuwa Raila Odinga, kiongozi wa ODM, alimtuma kwa mganga mwaka 2017 baada ya kumuomba ushauri wa kisiasa.
Barasa alisema alishangazwa sana alipoenda kutafuta ushauri wa kisiasa kwa Raila, lakini badala yake alimtuma Nigeria kwa mganga.
Alisema hilo lilimfanya kuachana na kusaka tiketi ya ODM na badala yake akaingia Jubilee ambapo aliishia kupata ushindi.
Barasa alisema ana ushahidi kuonyesha kuwa Raila hutegemea nguvu za kishirikina kwa manufaa ya kisiasa.
Alisema Raila alimpa ushauri wa kishirikina ili kushinda uchaguzi 2017.
Barasa alijipata pabaya wakati wa uchaguzi wa Kibra Novemba 7 baada ya kushambuliwa na kundi la vijana waliokuwa wameandamana na mbunge wa Dagoretti Kaskazini Simba Arati.
Alisema hatua hiyo ilimshangaza kwani wamekuwa marafiki na Arati tangu siku zao kama viongozi wa wanafunzi.