This archive report was first published on 15 November 2019.
Rais Uhuru Kenyatta anatarajiwa kufanya kikao cha faragha na wabunge wa Mt. Kenya kuanzia asubuhi Ijumaa, Novemba 15, 2019, katika Sagana State Lodge.
Mkutano huo unajiri siku chache baada ya Rais kupangua safari ya ziara katika kaunti ya Murang'a Jumapili, Novemba 10, 2019, ambapo alihudhurie ibada ya kanisa katika eneo la Kenol.
Mkutano huo pia unajiri wakati ambapo kuna joto la kisiasa kuhusu Jopo la Uwiano BBI na pia mgawanyiko ndani ya serikali ya Jubilee.
Chama cha Jubilee kimegawanyika katika mirengo ya Kieleweke na Tangatanga, na wabunge wanaoegemea upande wa DP Ruto wanahofia kuwa huenda wakakemewa na Rais.
Kufikia Alhamisi, Novemba 14, jioni, kulikuwa na ripoti kuwa wabunge waliokuwa wamealikwa ni wale wa mrego wa Kieleweke ambao unajipigia debe kwa kusema unaunga mkono Rais na mwafaka wake wa Handisheki.
Wafuasi wa Tangatanga, ambao ni wandani wa Naibu Rais William Ruto, walikuwa na wasiwasi kuwa huenda Rais atatumia mkutano huo kuwakemea kutokana na siasa wanazoendesha za kumpigia debe DP.