Skip to main content

Mwanamke Afariki Akijisaidia Baada ya Choo Alimokuwa Kuporomoka

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 14 November 2019.

Mwanamke mwenye umri wa makamo alifariki katika kijiji cha Uthiini, kaunti ya Machakos, mnamo Jumatano, Novemba 13, 2019, baada ya choo alimokuwa akijisaidia kuporomoka.

Alifariki papo hapo kwenye kisa hicho kilichotokea majira ya asubuhi, kwa mujibu wa mama mkwe wa marehemu Mary Nyiva.

Alisikia sauti kubwa nje majira ya asubuhi nikiwa chumbani, na alipotoka nje kuangalia kilichokuwa kimetokea, alibaini kuwa binti yake mkwe alikuwa ametumbukia chooni na kufariki papo hapo.

Aliondolewa chooni humo na mwili wake ulisafirishwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha Kagundo hospital.

Maporomoko ya vyoo hayo yanadaiwa kusababishwa na mvua kubwa inayoendelea kunyesha katika eneo hilo, na kulegea kwa sakafu za vyoo.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →