This archive report was first published on 14 November 2019.
Polisi wamepata bastola iliyokuwa imefungwa ndani ya chupi na kuachwa katika kichaka karibu na daraja la Isiukhu, Kakamega, mnamo Alhamisi, Oktoba 14, 2019.
Naibu kamanda wa polisi eneo la Shinyalu Moffat Museti alisema kuwa, majangili waliokuwa wakisakwa na maafisa waliiacha bunduki hiyo mbayo inasemekana walikuwa wakiitumia kutekeleza uhalifu kaunti ya Kakamega na viunga vyake.
Polisi wameapa kuwasaka majangili hao na kuwachukulia hatua kali za kisheria.
Wakati wa kushiriki habari hii, Mwenyekiti wa Nyumba Kumi Hussein Muhanji Alusa, wakishirikiana na polisi, waliwafumania majambazi hao katika kichaka hicho na kupelekea kwao kutoroka na kuiwacha bastola hilo.
Alusa alisema kuwa watu wengi wameripotiwa kuuawa na majangili hao ambao hutekeleza uhalifu wao katika daraja hilo kwenye barabara ya Kakamega kuelekea Kisumu.