This archive report was first published on 12 November 2019.
Mwenzetu Njenga Mswahili alikuwa na msongo wa mawazo, alitaka msaada lakini hakuna aliyemsaidia - Eric Omondi ¶
Eric Omondi amesikitika na kusema jinsi mchekeshaji wa Churchill show, Anthony Njenga Mswahili alivyokuwa akisumbuka.
Alipatikana ameaga dunia Alhamisi, Novemba 7, eneo la Soko la Ndonyo mtaani Dagoretti South, na anadaiwa kugongwa na treni.
Eric Omondi anasema Njenga Mswahili alikuwa na msongo wa mawazo na alitafuta msaada lakini hamna aliyemsaidia.
Alisema wengi walifahamu kuhusu hali ya Mswahili na kifo chake kimemuumiza kwa kuwa alishuhudia kikimfika kuanzia miaka mitatu.
"Njenga alikuwa anatuilia lakini sote - nikiwamo, hatukumsaidia, ni kama hatuna utu tena," alisema Omondi.
Ingawa kifo cha Mswahili hakijafahamika vyema kilitokea vipi, kuna madai kuwa huenda alijiua kutokana na matatizo aliyokuwa akiyapitia.