This archive report was first published on 11 November 2019.
Wanafunzi 18 wa shule ya upili ya Kobala Mixed waliwahi kupatika kwenye klabu huko Rachuonyo, baada ya kupataa kiuno. Wanafunzi hao waliachiliwa baada ya wazazi wao kufika.
Chifu wa eneo hilo Peter Agunga alidhibitisha kisa hicho na kusema kuwa wanafunzi hao waliingiwa na utukutu licha ya kuwa ni watahiniwa.
"Usimamizi wa shule umedhibitisha kuwa wote ni watahiniwa. Waliruka kwenye ua la shule hiyo ili wasijulikane na toweka," chifu Agunga alisema.
Wanafunzi hao ni watahiniwa wa KCSE na walitoweka shuleni na badala yake kwenda burundani.
Chifu huyo alisema alipewa ripoti kuhusu kisa hicho na raia na ndipo akatafuta maafisa wa polisi waliowatia mbaroni wanafunzi hao.
"Nilipata simu kutoka kwa wananchi na ndipo nikaelekea walipokuwa wanafunzi hao kabla ya maafisa wa usalama kuja na kuwatia mbaroni," aliongeza.