Skip to main content

Mwanga wa Kiswahili: Stadi za Lugha

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 11 November 2019.

Stadi za lugha ni muhimu sana katika maisha ya mtu yeyote. Kusoma ni jambo la maana sana ambalo hupanua akili na mawazo ya mtu sana.

Shule zimefungwa na wanafunzi wako likizoni ambayo ni ndefu zaidi ya wiki tisa. Lakini, kuna maswali mengi kuhusu stadi za lugha katika shule hizi.

Je, wanafunzi na walimu wanafanya nini ili kujiboresha kilugha? Hapana siku mwalimu hata mwanafunzi atakuwa bora katika lugha yoyote bila kusoma vitabu aula.

Utafiti unaonesha kuwa asilimia kubwa ya Wakenya hawapendi kusoma vitabu. Hili nimethibitisha baada ya kutembelea shule mbalimbali nchini.

Ukiuliza mwanafunzi akutajie kitabu chochote cha hadithi au riwaya atakutajia vile ambavyo hutahiniwa shuleni hapana zaidi ya hivyo. Msiba! Kwa nini wanafunzi wetu hawapendi kusoma? Labda ni uzembe au mapuuza au niseme kasumba potovu.

Leo, tunauliza wale walimu wasome vitabu ainati ili kujiimarisha zaidi. Hili litapevusha akili na fikra zetu.

Na kwa nini, usome zaidi vitabu ili kuwa bora katika lugha. Utaboreka ukisoma. Hii likizo iwe ya kusoma, kusoma na kusoma.

Makala yameandikwa na Sakwa Titus, mwalimu na mwandishi wa Kiswahili.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected]; [email protected] au WhatsApp: 0732482690. Tufuate kwa Telegram: Tuko news.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →