This archive report was first published on 10 November 2019.
Mbunge wa Kibra, Didmus Barasa, alishambuliwa na wahuni wakati wa uchaguzi mdogo wa Kibra ulioandaliwa majuzi. Mbunge wa Suna Mashariki, Junet Mohammed, ametangaza kuwa amepata kofia ya Barasa ambayo ilikuwa imepotea wakati wa purukushani hiyo.
Junet Mohammed alisema alikuwa kwenye harakati ya kukagua chumba cha Raila ndipo alipata kofia hiyo ambayo anadai atahakikisha inamfikia mwenyewe.
Alisema atamrejesha kofia hiyo kwa Barasa kama ishara ya amani baada ya chama hicho kutwaa ushindi.
"Nimekuwa nimekita kambi hapa tangu kura ilipoanza na nilikuwa nikikagua chumba cha Raila ambapo nilipata kofia ya mwizi aliyekuwa akijaribu kuiba chumbani," alisema Junet.
Barasa alishambuliwa na wahuni waliochochewa na Mbunge wa Dagorretti Kaskazini, Simba Arati ambaye aliwaagiza vijana hao kumtimua.
Arati alijitetea kwa kusema kuwa aliokoa maisha ya mwenzake kinyume na kile kilichoonyeshwa kwenye video.
Alisema alimuokoa kwa sababu vijana hao huenda wangemudhuru Barasa.
Arati pia alikuwa mwepesi wa kusema atakabiliana na mwanasiasa yeyote ambaye atahusika katika wizi wa kura.