Skip to main content

Wazee wa Kaya wamfanyia Gavana Mike Sonko matambiko

N

Nyakundi Report

Newsroom 2 min read

This archive report was first published on 10 November 2019.

Wazee wa Kaya wamfanyia Gavana Mike Sonko matambiko

Wazee wa Kaya wamefanya matambiko kwa Gavana Mike Sonko, wakiomba Mungu kumlinda dhidi ya matapeli.

Wazee hao waliandamana hadi eneo takatifu la Kaya Kinondo, Msambweni, mnamo Jumamosi, Novemba 9, ambapo walifanya maombi maalum iliyoambatanishwa na densi ya kitamaduni huku wakiomba miungu kumlinda Sonko.

Wazee hao walikuwa wamevalia mavazi ya tamaduni ya Kaya, na walishikilia kuwa wale ambao wanampiga vita Sonko walimuonea wivu kwa sababu ya rekodi yake ya maendeleo na kutishia kuwalaani endapo wataendelea kumsumbua 'mtoto wao'.

"Gavana Sonko ni mtoto wetu. Tulimlea hapa Kwale. Huwa tunawalinda watoto wetu. Ndio maana tutamlaani yeyote ambaye atajaribu kumdhuru," alisema mzee Abdalla Mnyenze, Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa Mijikenda.

Wazee hao walimuomba Rais Uhuru Kenyatta kumlinda Sonko dhidi ya mahasidi wake kwa sababu ya kumsaidia kupigana na ufisadi katika kaunti ya Nairobi.

"Kama wewe tu (Uhuru Kenyatta) umekuwa ukikabiliana na ufisadi, ni sawa na Sonko. Unatakiwa kumlinda kijana wetu," alisema Mnyenze.

Maombi hayo yalifanywa baada ya Sonko kuhudhuria ofisi za Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi (EACC) mara nne sasa chini ya miezi miwili, huku akishikilia kuwa maafisa hao walitaka kujua endapo aliwahi kushtakiwa.

Maombi hayo yalifanywa pia baada ya Sonko kuingia katika kundi la vijana wenye hamaki ambalo lilizua vurugu wakati wa mahojiano hayo, huku akishikilia kuwa alitembelea ofisi ya EACC akiwa pekee yake lakini wafuasi wake ndio walijumuika pamoja na kumfuata ili kufuatilia mahojiano hayo.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →