Skip to main content

Shule ya Msingi Australia inaunga mkono Eliud Kipchoge katika Kampeni ya Daily Mile

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 10 November 2019.

Shule ya Msingi kutoka nchini Australia, Tweed Heads Public, imegusa mioyo ya Wakenya baada ya kutumia jina la Eliud Kipchoge kama kauli mbiu yake ili kuunga mkono mpango wa Daily Mile.

Shule hiyo, kupitia ukarasa wao wa Facebook, ilikubaliana na kampeni ya bingwa huyo kwa kubatilisha kauli yao kuwa, No Human is Limited Eliud Kipchoge.

Shule hiyo ilipachika picha hiyo huku ikisema: "Habari Eliud?, Salamu kutoka kwa shule yetu nchini Australia. Kampeni ya Daily Mile ni wazo nzuri sana!"

Shule ya Msingi hiyo inaunga mkono Eliud Kipchoge katika kampeni ya Daily Mile, ambayo inalenga kuwasaidia wanafunzi wa shule za msingi kuanzia chekechea kuimarika kiafya.

Wanafunzi hao wanatakiwa kukimbia kwa pamoja kwa muda wa saa 15 huku wakipumua hewa safi.

Published on November 10, 2019

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →