This archive report was first published on 9 November 2019.
Mchungaji wa Abuja anawalipisha waumini KSh 14k kuogelea katika bwawa lake la maji matakatifu ¶
Uchungaji wa Abuja alijenga bwawa la kuogelea ndani ya kanisa lake, ambalo linatambulika kama Bwawa la Bathsheba. Bwawa hilo linaaminika kuwa na maji matakatifu ya uponyaji.
Alidokeza kuwa mchungaji huyo anawalipisha waumini wake KSh 14,000 (N50,000) ili kuogelea katika maji hayo.
Wale ambao hawana hela za kuogelea, wanalazimika kulipa KSh 2,830 kuchotewa maji hayo kwenye chupa.
Ujumbe huo ulichapishwa na Kelvin Odanz kwenye mtandao wa Twitter.
Odanz alidai kuwa mchungaji huyo alitengana na mkewe na kumuoa mpango wake wa kando.
Aliongeza kuwa angependa sana kufichua jina la mchungaji huyo na kanisa hilo ila hataki kuadhibiwa na Mungu.
Odanz alifichua kuwa kanisa hilo limejengwa eneo la Kubwa.