This archive report was first published on 9 November 2019.
Uchaguzi Kibra: DP Ruto adai Raila alitumia makundi haramu kupata ushindi ¶
Naibu Rais William Ruto amemkabili kinara wa ODM Raila Odinga kwa kutumia makundi ya haramu kupata ushindi katika uchaguzi wa Kibra.
Alisema kuwa Raila hakuna sera za kushinda kura kando na kutumia makundi ya haramu ili kupata ushindi.
Alisikitika kuwa Raila hakupata funzo lolote kutokana na salamu za maridhiano baina yake na Rais Uhuru Kenyatta.
Uchaguzi wa Kibra ulikumbwa na machafuko ya aina yake huku wafuasi wa Jubilee na viongozi wakiwa waathiriwa wakubwa.
Aliyekuwa seneta wa Kakamega Boni Khalwale, mbunge wa Lang'ata Nickson Korir, Oscar Sudi (Kapsaret), Charles Jangua (Starehe) na Didmus Barasa (Kimilili) walikuwa tu baadhi ya viongozi wa Jubilee ambao walishambuliwa na vijana.
Imran Okoth wa ODM alitangazwa mshindi baada ya kupata kura 24,636 dhidi ya 22,200 za McDonald Mariga wa Jubilee.
Naibu Rais William Ruto amemkabili kinara wa ODM Raila Odinga kwa kutumia makundi ya haramu kupata ushindi katika uchaguzi wa Kibra.