This archive report was first published on 8 November 2019.
Tharaka Nithi: Mzee Awagombeza Vijana Wake Kwa Kuoa Mabibi Wengi ¶
November 8, 2019
Mzee kutoka eneo la Thiiti, Tharaka Nithi, alikuwa na tabia ya kuwagombeza vijana wake kwa kuoa wanawake wengi bila mpango. Kwa mujibu wa Taifa Leo, buda huyo mwenye vijana saba alijitahidi kuwapa wanawe hao malezi bora na kuhakikisha kuwa wamepata masomo.
Walipotimia umri wa kuoa, vijana hao hawakufanya vyema katika masomo na walikuwa hawana chochote, ikamlazimu baba yao kugharamika kuwalipia mahari.
Aliwapa miezi miwili kwa kila mmoja wao kujipanga jinsi ya kujukumikia familia zao, na wakati uo huo alitoa makataa ya mwake mmoja kwa kila mmoja wao kuhama katika boma lake na kujitafutia mahali pengine.
Wazee wenzake walimuunga mkono na kuwasuta vijana hao kwa kuidhoofisha afya ya mzee kwa kumtundika mizigo yao na familia zao.
Aliwakemea vikali kwa kumpa presha na kwa kuleta wake zaidi ya mmoja na kumuongezea gharama zaidi ya kulisha familia zao.
Aliwataja kwa kikao na wazee wa kijiji, akisema, "Nimejitahidi kwa udi na uvumba kuwasomesha na kisha kuwalipia mahari mkapata wake. Mbona msiende huko mjini kutafuta ajira kama jirani wenzenu, au hata mfanye vibarua ili kuwakimu wake zenu? Nitaendelea kuwalisha hadi lini?"